|
Hatua saba za kukamilisha taarifa bora kwa ajili ya mradi wako wa mazingira zinajumuisha:
Tupe habari kuhusu kikundi chako, jina ya mradi nakadhalika najinsi ya kuwasiliana nawewe mradi wako ukiingizwa fainali.
Tueleze madhumuni ya mradi wako, na tatizo la kimazingira unalotaka kutatua. Kwanini uliuchagua mradi huu? Umeufanyia kazi kwa muda gani?
Nini matarajio yako – matokeo yepi ya mradi yatakayo tatua tatizo? Yana manufaa gani au yatakuwa na manufaa gani kwenye eneo lako?
Waamuzi wa shindano wanazingatia shughuli ambazo zinaonyesha umuhimu wa mradi wako. Ulifanya vipi utafiti kuhusu umuhimu wa mradi wako? Elezea utafiti ulioufanya kama chanzo cha mradi wako. Hali ilikuwaje kabla hujaanza? Ulipata ushirikiano gani toka kwa uongozi katika jamii, kampuni binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na watunga sera?
Mpango kamili uwe na orodha ya kazi za vitendo ambazo zimetekelezwa au zitatekelezwa na kikundi ili kufikia malengo yanayo tarajiwa. Kazi hizo zaweza kuwa ni za vitendo halisi kama vile kupanda miti au zaweza kuwa ni za kimawasiliano, kama vile uzinduzi wa kampeni kwa kutumia vyombo vya habari na mabango au kuandika sera za kuboresha mazingira na kuziwasilisha kwa uongozi wa jamii. Iwapo kikundi kina mapendekezo kwa mamlaka husika au kampuni basi nayo pia yaingizwe. Waamuzi watakua wakitafuta ushahidi wa hatua iliyochukuliwa na manufaa yake.
Hii ieleze dira na malengo ya uboreshaji wa mazingira. Kwa mfano, ni kwa kiasi gani kikundi chenu kinadhani matumizi ya maji au nishati katika shule yenu yapunguzwe? Mnapimaje mafanikio yenu? Jamii yenu imepata manufaa gani kwa uanzishaji wa mradi huu? Ni nani wanashiriki na kuwasaidia? Ikiwa mradi umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa, mmepimaje mafanikio yake?
Kwenye sehemu hii elezea kwa kifupi chanzo, malengo ya mradi, shughuli zilizofanyika na matokeo yake. Mara umalizapo hatua zote wasilisha kwenye tovuti. Miradi ile tu itakayowasilishwa kwa kutumia mfumo ufuatao ndiyo itafikiriwa na waamuzi. Sasa ingia uwanjani!
Projects must be submitted in English!
|